Popular Post

Posted by : ujugu Alhamisi, 8 Mei 2014

Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni amelezwa toka jana katika hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa Dengue.
Akizungumza na Bongo5 leo Dr Cheni amesema kuwa bado hali yake sio nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili kupoteza nguvu.
“Bado ni nipo hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui unaitwa Dengue,” amesema. “Bado hali yangu sio nzuri kabisa,yaani naumwa,napungukiwa damu,mwili unauma,kwahiyo yanai bado ninaumwa,hii homa ilinianzia wiki iliyopita sema nilikuwa bado hawajaigundua ila jana ndio wameingundua,” ameongeza.
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba Watanzania wamuombee kwani bado hali yake sio mzuri.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

comment

- Copyright © MKWERE ORIGINAL - m.media - Powered by Blogger - Designed by M.MEDIA haji mabovu -