Popular Post

NMB YAWAFIKIA WANA KONGWA: YAFUNGUA TAWI JIPYA KIBAIGWA-KONGWA, DODOMA

By : ujugu

NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa –Dodoma. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote.
Tawi la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai.
Kufunguliwa kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa NMB wa eneo hilo wa kupata tawi lenye nafasi ya kutosha .Aidha  eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wakubwa wa NMB na wananchi kwa ujumla .
Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii, benki ya NMB inatoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya hospitali na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Kibaigwa kwa kuendelea kwao kuunga mkono maendeleo ya benki.
NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 150, ATM Zaidi ya 500 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia Milioni mbili hazina ambayo hakuna benki yenye nayo.

 Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai ,akiweka sahihi
kwenye kitabu cha wageni mara tu baada ya uzinduzi wa Tawi la NMB kibaigwa .
Hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo umefanyika jana katika viwanja vya Tawi la NMB Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoni Dodoma
 Sehemu ya wageni Waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
 Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai  akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kibaigwa
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai (Kati kati)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kibaigwa.

Professor Jay Afungua Website Yake,Link Ipo Hapa

By : ujugu
PROF jayRapper Profesa Jay amefungua website yake ambayo itakuwa ikitoa taarifa tofauti kuhusu maisha yake na muziki wake. Website hii itakuwa na picha za matukio yote kuhusu Profesa Jay na kama wewe ni shabiki basi itakuwa chanzo chako cha habari za msanii wako.
Website hii ni  www.profesajay.com  Bonyeza Kwenda moja kwa moja.

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya Falcao kuhamia Man United

By : ujugu

IMG_6950.JPGUsiku wa jana klabu ya Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo.

Falcao ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vya Arsenal na Man City amejiunga na Man U akitokea klabu ya Monaco ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico Madrid.
Usajili wa mchezaji umezungumzia na watu wengi mmoja wao ni mchezaji bora wa ulaya na dunia – Cristiano Ronaldo.
Akiongea jijini Madrid Ronaldo alisema: ‘Falcao ni mchezaji mzuri sana, nadhani Manchester United wamefanya jambo zuri kumsajili. Sidhani kabisa kama ni mchezaji asiyewafaa, ni mchezaji wa daraja la dunia na hivyo naamini huu usajili mzuri.”
Tag : ,

Walichokisema wazazi wa wasichana waliotekwa Nigeria.

By : ujugu
wazaziWazazi wa wasichana waliotekwa nyara nchini Nigeria wamekanusha madai kuwa wanaingiza siasa kwenye kilio chao kuitaka serikali ya nchi hiyo iwaokoe watoto wao.
Hii ni baada ya wazazi hao kukataa wito wa kukutana na rais Goodluck Jonathan hapo jana baada ya kushinikizwa na mwanaharakati mdogo kutoka Pakistan Malal Yousafzai.
wazazi2
Rias Jonathan amesema ni aibu kubwa kwa wazazi hao kuruhusu kushinikizwa na mitandao ya kijamii hasa kutokana na kampeni yao kwenye mitandao yenye kauli mbiu, “Bring Back Our Girls”.
Lakini msemaji wa wazazi hao, amesema kuwa walikataa kukutana na Rais kwa sababu jamii ya watu wa Chibok haikuwa imewapa ruhusa kufanya hivyo.

Kuhusu mama aliyemtelekeza mtoto wake ndani ya karatasi.

By : ujugu

mtotoo


Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, Mwanamke mmoja aliyemtelekeza mwanawe ndani ya karatasi ya plastiki katika bustani moja nchini Uingereza amenusurika na adhabu ya kifungo jela.
Mtoto huyo mchanga aliyekuwa wa siku moja tu, alikutwa na mtu aliyekuwa anamtembeza Mbwa wake katika bustani hilo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita na kuwekwa chini ya ulinzi wa maafisa wa kijamii kwa miaka miwili.
Hata hivyo alikiri kumtelekeza mtoto wake kwa makusudi na kusema kuwa aliathirika kimawazo baada ya kujifungua mtoto huyo mwezi Mei.
Polisi walisema kuwa mtoto huyo alinusurika kifo kwa dakika thelathini tangu kutelekezwa kwani alipatikana haraka sana na kwamba mwili wake tayari ulikuwa umeanza kuwa baridi.
Mtoto huyo alipatikana mwaka jana akiwa amefungwa ndani ya taulo na kuwekwa ndani ya karatasi ya Plastiki katika bustani hilo.
Mama huyo aliambia mahakama kuwa alifanya kitendo chake katika hali ya kutojielewa.
Pia alifahamisha mahakama kuwa alijifungulia mtoto wake katika sakafu ya bafu nyumbani kwa mamake hali ambayo ilimuathiri kimawazo.
Alificha ujauzito wake kutoka kwa familia yake na pia hakuwahusisha madaktari kwa sababu alihofia kuwa hangeweza kustahamili ujauzito wake.
Tag : ,

DIAMOND PLATNUMZ BET RED CARPET AND BEHIND THE SCENE !

By : MKWERE ORIGINAL


Diamond Platnumz akipita kwenye Red Carpet ya BET mbele ya Mapaparazi zaidi ya 200,Mwanamuziki huyu alionekana kuwavutia watu wengi na Suit yake iliyokuwa imemkaa kisawasawa ambayo waingereza wanasema  "Well Tailored Suit" By Designer Sheria Ngowi .
Mapaparazi zaidi ya 200 walichukua every step and moments za Red Carpet wakati Diamond akipita
Mwanamuziki Nelly alitushangaza pale alipomvuta koti Diamond kwa nyuma na kumwta kwa Jina,Tulishangaa sana kuona kumbe wanamuziki wa Marekani nao wanafatilia habari za African Nominees.
Hapa Diamond aligeuka nakukuta aliye mvuta koti ni Nelly ambaye alimwambia congratulations.
Ndani kwenye Award show Diamond na USA Manager wake  Bwana DMK wakipata Ukodaki

   Hapa Mwana Muziki Neyo alimwita Diamond wakati akipita Nakumwambia Congratulation jambo ambalo lilitushangaza kuona kumbe hata wanamuziki wamarekani wamefatilia sana habari za wanamuziki waliokuwa nominated kutoka mataifa ya Africa.
 Behind The Scene Diamond akiwa na Super Designer aliyedesign Suit ya Diamond -Mr Sheria Ngowi.
Picha hii ilipgwa kutika angani vile
 Diamond akiwa na USA Tour Manager wake Bwana DMK akifanyiwa Interview kwenye Red Carpet
Behind the scene Diamond akihojiwa na Factory 78 ya UK
Behind the Scene Diamond katika Picha ya Pamoja na DMK ambaye ndiye USA Tour Manager wake
Diamond akihojiwa na Karrueche Tran Kwenye Red Carpet (Karrueche ni Girlfriend wa Chris brown)

Singer Faith Evans ambaye ni Mke wa Marehemu BIG alipata nafasi yakupiga picha na Diamond

Camrea yetu ilimpata Platnum katika poz hili

Picha iliyotamba kwenye Blogs za marekani jana -Diamond katika Poz la Kisheria Ngowi

Diamond akihijiwa na XXL magazine kwenye RED Carpet pembeni yake ni USA Manager DMK

Mtangazaji wa Fox Entertainment akimuhoji Diamond kwenye Red Carpet


RexEnergy

Kauli ya TID kwa Ray C na alichokisema baada ya kuibuka maswali juu ya kauli hiyo.

By : MKWERE ORIGINAL


RexEnergy
1170077_216447715233225_272121298_n
June 30 kupitia mtandao wa kijamii wa instagram kwenye akaunti ya Tid alipost picha iliyokuwa na maneno >>’Listen to this mix….once again from @lamarfishclub’ ni wimbo ambao ameurudia kwa mtindo anaoufanya Lamar kwa sasa zile Refix.
Baada ya kuweka picha hiyo mmoja wa watu waliotoa maoni yao au comments kwa picha hiyo ni mwanamuziki Ray C ambaye aliandika maneno haya yaliyooneka kumkera TID
tid
Ray C ameandika “Come let’s talk Tid u are the best musician in East Africa please lets talk” maneno haya hakuna aliyejua Ray C anachomaanisha lakini cha kushangaza na ambacho kimeibua maswali ni jinsi TID alivyojibu comment hiyo.
Leo kupitia kipindi cha Xxl Tid ameelezea sababu ya kuandika hivyo ambapo amenukuliwa akisema “Mimi kama kuna mtu ananitafuta hawezi kunitafuta kwenye instagram, sijawahi kuwa na matatizo na Ray C sijamuona nina kama miaka 5 hivi”
“Hivi Ray C anataka kukutana na mimi nini anataka kuongea na mimi mbona hajanitafuta miaka yote ananitafuta sasa hivi mimi sijapenda sasa nakutuma wewe mwambie jamaa hataki kuonana na wewe”
“Sitaki kuongea nae, sitaki kukutana nae akaongee na ma boyfriend wake ambao anafanya nao vitu vibaya, mimi si wa namna yake aniache na familia yangu anaiche na mama yangu”.
Bonyeza play kusikiliza alichokisema zaidi Tid.

taarifa kuhusu ndege iliyodondoka alfajiri ya July 02 Kenya.

By : ujugu

254

Taarifa kutoka Kenya naambiwa watu wanne waliokua kwenye ndege iliyokua ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi kuelekea Mogadishu Somalia wamefariki dunia baada ya Ndege hiyo kuanguka katika eneo la Utawala dakika chache baada ya kupaa,
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya July 02 na inaaminika kwamba ndege hiyo ilikua iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa zinginezo kuelekea Somalia.
Walinzi wawili walijeruhiwa mmoja ametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku mmoja amelazwa katika hospitali ya mama Lucy,kwa mujibu wa mkuu wa polisi Jijini Nairobi Benson kibue amethibitisha ajali hiyo na kusema kuwa Ndege hiyo yenye nambari 5Y-CET ilianguka kwenye paa la jengo la kibiashara likijaribu kutua ghafla na kushika moto papo hapo likiteketeza watu wanne waliokua ndani.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kwenye mabaki ya ndege hiyo kuona iwapo kuna waasika zaidi.

Watanzania Tunaweza,Mengi akavaa jarida la frobes Africa july 2014

By : ujugu

barefoot to $550 milion ndio maneno yaliyoko kwenye picha ya mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya ipp media iliyopo kwenye cover la forbes africa litakalo tolewa july mwaka huu kwenye jarida hilo mengi ameeleza tangu alipo kuwa anatembea peku hadi kuwa na utajiri wa dola milioni 550

Wabunge Waumbuana Kupokea Rushwa Bungeni

By : ujugu

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga (Chadema), amewaumbua wabunge wenzake kuwa wanapeana na kuchukua rushwa ndani ya Bunge.
Suzan aliyasema hayo juzi jioni wakati akichangia katika mkutano wa Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC). Suzan alisema vitendo hivyo vya rushwa vilionekana wakati wabunge hao walipokuwa wakiwachagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
“Rushwa ilikuwa ni wazi wazi ukienda chooni unapewa laki mbili (Sh200,000) unaondoka,”alisema Suzan.
Alisema wao kama viongozi ambao wanatunga sheria na wanatakiwa kuisimamia serikali wanapaswa kuwa waadilifu. Hata hivyo, Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), alisema hakuna ukweli kuhusu jambo hilo la baadhi ya wabunge kuchukua rushwa hadi chooni.
Hata hivyo, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura (CCM), alimuunga mkono Suzan na kusema suala hilo ni la kweli na kwamba kama Sanga hakuliona walikuwa wanamkimbia.
“Alichokizungumza Suzan ni cha kweli. Kaka yangu (Sanga) walikuwa wanakukimbia. Ni kweli hilo lilifanyika,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa APNAC, Vita Kawawa, alisema si vyema wabunge wenye taarifa kuhusiana na masuala ya rushwa wakatoa taarifa katika ofisi za Spika na kamati ya maadili ili liweze kufanyiwa kazi mara moja.
“Ni vyema mkatupa taarifa kitu ambacho kinaashiria rushwa sisi tupo, ofisi ya spika ipo na kamati yetu ya maadili,”alisema.
Alisema rushwa ni mdudu ambao unatakiwa kukataliwa na kila mtu. Alisema rushwa imesababisha maisha ya wananchi kutobadilika ingawa uchumi wa nchi unakuwa.
Tag : ,

comment

- Copyright © MKWERE ORIGINAL - m.media - Powered by Blogger - Designed by M.MEDIA haji mabovu -