Popular Post

Posted by : ujugu Alhamisi, 15 Mei 2014

Producer mkongwe wa muziki na mmliki wa MJ Records, Master J, amesema uchawi upo kwenye muziki na ameshawahi kushuhudia msanii wa bendi akitolewa panzi kooni iliyoingia kimazingara ili ashindwe kuimba.
Akiongea na kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio jana, Master J amesema wapo baadhi ya wanamuziki wanaojihusisha na masuala ya ushirikina.
“Hivi ni vitu vya kawaida, huu ni utamaduni wetu,mimi sishangai wala sioni kitu chochote cha ajabu. Mimi nilianza kwa kurekodi muziki wa rap tu, lakini baadaye nikaanza kurekodi band, Taarab na mchiriku ndio maana nishasemaga nimeshawahi kuona kwenye band mtu anatoa panzi kabisa kutoka kooni, akafanyiwa maujanja ndo akaweza kuimba. Kusikia wasanii wa Bongo Flava wanajihusisha sio kitu cha ajabu kwani wao si ni Watanzania na Tanzania taka usitake utamaduni wetu ni uchawi, uchawi upo,kwahiyo mimi sishangai,” alisema.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

comment

- Copyright © MKWERE ORIGINAL - m.media - Powered by Blogger - Designed by M.MEDIA haji mabovu -