Popular Post

Archive for Agosti 2013

KAMA HUKU BAHATIKA KUONA PIICHA HIVI NDIVYO SAMAKI SAMAKI ILIVYOTEKETEA KWA MOTO HUKO MBEZI...

By : MKWERE ORIGINAL


Baada ya thesuperstarstz kufika eneo la tukio lilifanikiwa kuona jinsi askari wa zima moto walivyokuwa wanajitaidi japo walishachelewa kwani moto ulishateketeza eneo lote . Makachero  wa thesuperstarstz wakiwa eneo hilo la tukio walianza kumsaka mmiliki wa eneo lile ambae ni raia wa kigeni na alipopatikana alisema kwasasa hana chakuongea kwani hasara aliyoipata ni mungu tua ndio anajua


Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakiendelea kuzima moto ulioteketeza baa ya Samaki Samaki iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwananchi akichukua baadhi ya matukio wakati moto ukiteketeza baa ya Samaki Samaki.

wananchi wakiangalia kwa umakini tukio zima wakati moto ukiteketeza baa ya Samaki Samaki.
Zimamoto wakitafakari jinsi ya kuzima moto huo.
Zimamoto wakizima moto katika gereji ya Xenco iliyopo jirani na baa iliyoteketea.
Wananchi wakishuhudia zoezi la uzimaji moto katika baa ya Samaki Samaki 
Tag : ,

TAZAMA PICHA 15 ZA SHEREHE YA HAKIKA YA MTOTO WA MKWERE NTUMBANI KWAKE KIMARA-BONYOKWA

By : MKWERE ORIGINAL

MSANII WA MAIGIZO TANZANIA HEMEDI MALIYAGA AFANYA SHEREHE YA HAKIKA YA MTOTO WAKE SHAMSA HEMEDI MALIYAGA HUKO NYUMBANI KWAKE KIMARA-BONYOKWA

                                   SHAMSA HEMEDI MALYAGA



 MKE WA MKWERE NA MTOTO WAKE KAMIRA MWENYE IJABU NA SHAMSA AKIWA AMEMBEBA NA HUYO MWENYE JEZI YA YANGA NI MTOTO WA MPIGA PICHA KUTOKA ITV NOEL KAPANDA

   MKWERE NIKIWA NASIKILIZA DUA KUTOKA KWA SHEKHE HAPO PEMBENI YANGU
 
   NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WAKIWA NA MTOTO WANGU
 WAZEE WA FAMILIA YA MALIYAGA WAKIWA KWENYE POZI LA KUPIGA PICHA
             MKWERE AKIWA NA MWANAE NYUMBANI KWAKE KIMARA
               SHAMSA HEMEDI MALIYAGA AKIWA KWENYE POZI
 MKWERE AKIWA NA MAMA MKWE,MKEWE NA MTOTO WAKE KAMIRA                  NA             SHAMSA ALIE BEBWA
         WADAU WAKARIBU WA MKWERE WAKIPATA CHOCHOTE KITU
                       WAMAMA WAKIFANYA YAO KWENYE MAHANJUMATI
                                  KAMIRA MTOTO WA MKWERE WA KWANZA

 

MWANAMKE AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMCHOMA MOTO AKIMTUHUMU KUWA NI MWIZI HUKO MPANDA

By : MKWERE ORIGINAL


Mzozo wa wapenzi wawili usiku, umesababisha mmoja wa kike kupiga mayowe ya kumuita mwenzake mwizi, akavamiwa na watu waliompiga na kumchoma moto hadi kufa.



Kisa hicho kimetokea mkazi wa Magazini mjini Mpanda mkoani Katavi, Florence Mabuga (29), ambaye baada ya kuvamiwa na watu akidhaniwa mwizi, alipigwa na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto mbele ya nyumba yake.



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amethibitisha kuuawa kwa mkazi huyo katika kisa hicho kilichotokea katika mtaa wa Nsemulwa-Magazini hivi karibini, usiku wakati Mabuga akimsindikiza mpenzi wake wa kike akitokea nyumbani kwake.



Akisimulia mkasa huo wa kusikitisha, Kamanda Kidavashari alisema Mabuga ambaye alikuwa msimamizi wa vibarua wa kujenga nyumba mjini humo, siku hiyo baada ya kurejea nyumbani, alitembelewa na mpenzi huyo ambaye jina lake halijafahamika.



Inadaiwa wakati Mabuga akimsindikiza rafiki huyo, ulizuka mzozo baina yao ambapo Mabuga alitishia kuwa usiku huo angechoma nyumba ya rafiki huyo, ndipo kwa hasira na hofu ya kuchomewa nyumba, alipiga yowe akiashiria kuwa Mabuga ni mwizi.



Kwa mujibu wa Kidavashari, Mabuga alianza kutimua mbio mara alipoona kundi la wananachi wenye hasira wakiwa na silaha mbalimbali za jadi wakikimbilia alipokuwa amesimama na rafiki yake huyo.



Inadaiwa kuwa wananchi hao walifanikiwa kumkamata Mabuga aliyekuwa akijaribu kuingia ndani ya nyumba yake, na kuanza kumpiga na kumsababishia mauti.



“Uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa Mabuga alisingiziwa tu na mpenzi wake huyo, kwani hakuiba kitu chochote, ila mpenzi wake huyo alimpigia mayowe ya mwizi baada ya kuzuka mzozo baina yao,“ alidai.



Kwa mujibu wa Kidavashari mtuhumiwa huyo anaendelea kusakwa ili sheria ichukua mkondo wake, pia hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi sasa kwani wananchi hao walikimbia eneo la tukio mara baada ya kufanya unyama huo.
Tag : ,

TCRA YAJIPANGA KUZIFUNGA SIMU ZOTE ZA KICHINA ( SIMU FEKI )

By : MKWERE ORIGINAL


Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
 

Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kwa   kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya  zoezi la kuzima simu kuanza  ili  kuhakikisha kuwa   wananchi  hawaathiriwi  na  zoezi  hilo.
 
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.
 

-Bongo5
Tag : ,

AFYA YA MSANII MATUMANI IMEIMARIKA KIDOGO NA AMEREJEA TENA KATIKA FANI YAKE YA UIGIZAJI

By : MKWERE ORIGINAL




BAADA ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ hatimaye amepata nguvu na ameanza kujikongoja katika kazi ya uigizaji.
 
Akiongea na  mwandishi  wetu hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe.
  
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.
 
Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili yake jambo ambalo siyo la kweli.
Tag : ,

Vi2ko Mtaani

By : MKWERE ORIGINAL

Jamani haya maisha sijui nifanye nnili nipate RIZIKI maana dis tyme wananch hawatupi chakula kabsa kisa v2 vimepanda bei lol.
Dizan kama maza aninizingu hiv ye kila siku ananilazimisha kuoga sasa leo nammaliza kabisa yana ujinga wenyewe ukae kando
Sasa nyie leo ndio mtanitambua si hamtaki kucheza na mmm sasa leo mtacheza mtake msitake.
Umezidi kukaa UC*I wewe sasa inabidi tukuhifadhi

VITUKO NA VICHEKESHO USWAZI

By : MKWERE ORIGINAL

Jamaaa yupo kiabiashara zaidi na new style ya surual "DOUBLE BELT"
picha A                                       picha B 
Sasa hapo kwenye picha A ukiangalia kwa kukurupuka unaweza ukazan ki2 kinghine kabisa ambacho hakikualengo kamili la picha hiyo.
hapo sasa utata tupu kwenya picha B
Mambo ya uswahilini sasa Jamaa kashikwa UGONI anatembezwa UCHI mtaa mzima sasa hapo ndio utajua mke wa m2 sumu jamaa kawa mdogo kama piriton vle

{Vichekesho} Vituko vya Porini

By : MKWERE ORIGINAL

Porini nako vituko vitupu, hebu edekshie hii, siku moja panya katika tembea tembea yake si akamkanyaga nyoka. Mzozo ukawa kama ifuatavyo;Nyoka: Oya dogo mbona unanikanyaga?Panya: Dah, sory bro bahati mbaya.Nyoka: Bahati mbaya kitu gani, lione kwanza toto dogo midevu kibaoPanya: aaah nenda zako kule kubwa zima hadi leo linatambaa

{Vichekesho} Juma kavamia sherehe ya harusi ya wanyakyusa

By : MKWERE ORIGINAL

Jamaa mmoja aitwaye JUMA alivamia sherehe ya harusi ya wanyakyusa na kujifanya  mwanafamilia wa bwana harusi. Wakati wa utambulisho wa ndugu wa bwana harusi wakaanza kusimama mmoja mmoja na kutaja jina lake....

Wa kwanza akasema: Naitwa Mwakalebela
Wa pili akasema: Naitwa Mwakipesile
Wa tatu akasema: Naitwa Mwakasungura
Wa nne akasema: Naitwa Mwasomola
Wa tano akasema: Naitwa Mwakatundu
Ilipofikia zamu ya Juma akafikiriaaa kisha akadhani kuwa kila jina katika kabila lile ni lazima uanze na “MWA”, basi akainuka kwa makonfidensi na kupaza sauti “naitwa MWAJUMA

sasa mkwere orginal ipo hewani kwa matangazo kutokana na marekebisho ambayo wadau walita yabadilike

By : MKWERE ORIGINAL
kampuni ya mkwere original inapenda kuwatarifu wadau wake kuwa yale marekebisho ambayo waliyataka kuyaona kwanye blog hii sasa yamesha kuwa tayari kinachotakiwa sasa ni wao tu kutembelea. Kampuni ya mkwere inawependa wote na kuheshimu mawazo ya kila mtu na ndo maana tupo pamoja nanyi mpaka sasa asanteni na baadae

comment

- Copyright © MKWERE ORIGINAL - m.media - Powered by Blogger - Designed by M.MEDIA haji mabovu -